MAMBA MZITO ZAIDI MAREKANI ANASWA
 |
| Mamba aliyekamatwa Mississippi |
MAMBA mwenye uzito wa kg. 316
amenaswa kufuatia juhudi ya kumsaka iliyofanywa na watu wanne kwenye
ranchi ya Mississippi nchini Marekani na ameweka rekodi ya kuwa mamba
mzito zaidi nchini humo.
Eneo la chini la Mississippi Delta linahusisha klabu nyingi za uwindaji, ardhi ya mbao, kilimo na maeneo ya hifadhi za wanyama.
Rekodi ya awali nchini humo ilikuwa ni mamba mwenye uzito wa kg. 312 na alikamatwa mwaka jana kwenye maji hayo hayo ya Delta.
Mamba huyo ana urefu wa futi 13 na inchi 1.5.
Hata
hivyo, rekodi rasmi za mamba wakubwa zaidi duniani zinashikiliwa na
mamba wawili wenye urefu wa futi 20 (mita 6.2) na kg 1,200.
Mamba wa kwanza aliuawa Mto Mary
kaskazini mwa Australia mwaka 1974 na kupimwa na maafisa wa wanyama.
Mamba wa pili aliuawa mwaka 1983 katika Mto Fly, Papua New Guinea.
Katika suala la mamba wa pili, kilichopimwa kilikuwa ni ngozi ya mamba
huyo na inafahamika kwamba ngozi pekee huwa inatoa vipimo pungufu vya
urefu halisi wa mnyama, hivyo mambo huyo inawezkana alikuwa na urefu wa
sentimeta 10 zaidi.